Thursday 17 August 2017

Jini Mkatakamba Atua kwa Jenifer wa Kanumba Achafua Hali ya Hewa Mitandaoni.

MTOTO ‘mtukutu’ aliyejizolea umaarufu mkubwa kupitia filamu za marehemu Kanumba, Hanifa Daudi amekumbwa na kashfa ya kitapeli, kufuatia watu wasiojulikana kufungua akaunti feki ya jina lake kwenye Mtandao wa Facebook na Instagram na kuanza kuomba pesa kwa watu mbalimbali.

Kwa mujibu wa chanzo makini, baadhi ya watu wamekuwa wakimlalamikia  kwa tabia ya kuomba pesa kupitia mitandao ya kijamii, jambo ambalo liliwashangaza wengi. “Kuna watu wanatumia jina la Jennifer kwenye mitandao kutapeli hivyo wameondoa lawama kwa muigizaji huyo na badala yake wameanza kumkingia kifua, tofauti na zamani ambapo walidhani ni yeye kweli anayefanya utapeli huo, mwenyewe maskini amekuwa ni mtu wa kulia na kuumia kwa kashfa hiyo,” alisema mtoa habari wetu.

Mwandishi wetu alizungumza na Jennifer na kusema: “Naumia sana jamani, hebu nisaidieni, mimi sina akaunti kwenye Facebook, ni juzi tu mama yangu alinishauri nifungue akaunti ya Instagram ili kujitofautisha na hao matapeli, lakini sina simu na hiyo akaunti siitumii niko huku Tanga masomoni, wanatumia jina langu kutapeli, eti wanajiita Hanifa Jennifer Kanumba na wanaposti picha zangu, kweli sijui wanazitoa wapi, naumia jamani aah.”


Toa Maoni yako Hapa Chini:

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment