Wednesday 10 January 2018

Mrema Kudai Mabilioni ya Hela kwa Aliyemzushia Kifo.

Mwenyekti wa Bodi ya Parole nchini Mheshimiwa Agustino Lyatonga Mrema, amesema anaenda kufungua kesi ya madai ya mabilioni ya shilingi kwa watu waliomzushia taarifa za kifo hapo jana.


Akizungumza kwenye kipindi cha East Africa Breakfast kinachorushwa na East Africa Radio, Mrema amesema watu hao wamemletea tatizo kubwa sana la kushtua familia yake na watu wake wa karibu, hivyo anaelekea TCRA ili aweze kusaidiwa kuwabaini, na kuwapeleka polisi kuwafungulia kesi.

"Walivyotangaza jana Mrema amefariki kwanza nasikitika sana, kumtangazia mtu amekufa ni kweli nilihangaika jana, mke wangu alihangaika sana, watoto wangu, marafiki zangu wapenzi wangu walikuwa wanalia kwenye simu kufuatilia hizo habari kumbe ni uzushi, ni uongo habari za kijinga kabisa, nikitoka hapa sasa hivi naenda TCRA", amesema Mrema

Mrema ameendelea kwa kusema .."Nitakuwa kiongozi wa kwanza katika nchi hii kuchukua hatua kali, wanipe fidia inayostahili kwa kuniletea ujinga, nataka kujua huyu mtu aliyeanzisha huu uvumi na kuweka kwenye mitandao kwa ajili ya kunifedhehesha na kuniabisha, bilioni 20 wanilipe kwa usumbufu kwa aibu niliyopata jana".

Kwa upande mwengine Mheshimiwa Mrema amesema kitendo hiko kilimsaidia kujua ni watu gani wanampenda kweli na kina nani hawampendi, kutokana na reaction zao baada ya taarifa feki za kifo chake.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment