Tuesday 23 January 2018

RPC Aweka Wazi Sababu Kukamatwa Msigwa

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa, (RPC) Julius Mjengi amefunguka na kuweka wazi sababu zilizopelekea kumkamata Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na kudai kuwa walimkamata wakimtuhumu kuratibu kuchoma na kubomoa nyumba.


Mjengi amesema hayo leo Januari 23, 2018 wakati akiongea na www.eatv.tvna kudai kuwa Mbunge huyo jana alipokamatwa alihojiwa na baadaye aliachiwa kwa dhamana hivyo yupo huru kwa dhamana toka jana majira ya saa tano usiku.

"Jana Msigwa alijisalimisha baada ya kusikia tunamtafuta hivyo tulimuhoji na usiku alipata dhamana, hivyo sisi tulikuwa tunamtafuta kwa tuhuma za kuratibu matukio mawili ya uhalifu hapa Iringa Mjini ambapo kuna nyumba ya diwani mmoja ambaye alijiuzulu na kuhama CHADEMA na kuhamia CCM nyumba yake pagale lilibomolewa"

Kamanda aliendelea kusema kuwa 

"Lakini pia usiku wa kuamia tarehe 17 kuna nyumba moja Kihesa ilichomwa moto ikateketea na ndani mle katika wapangaji mmoja alikuwa ni Katibu wa UVCCM Wilaya ya Iringa Mjini kwa hiyo Msigwa ana tuhuma za kuratibu matukio haya, kwa hiyo tulimuhoji na kudhamini ila tunaendela naye" alisisitiza Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa, (RPC) Julius Mjengi  

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment