Saturday 13 January 2018

Kingunge arejeshwa Tena Muhimbili.

Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombare Mwiru amerejeshwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kuendelea na matibabu.

Kingunge aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo Januri 10, 2018 ili kwenda kushiriki tukio la mazishi ya mkewe ,Peras Ngombare Mwiru yaliyofanyika jana katika makaburi ya Kinondonbi jijini Dar es Salaam.

Pares alifariki dunia Januari 4, katika hospitali ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa ugonjwa wa kupooza huku Kingunge naye akilazwa hospitalini hapo akiuguza majeraha ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake, Victoria jijini humo hivi karibuni.

Mtoto wa Kingunge, Kinje Ngombare Mwiru  jana alisema baada ya baba yake kupata kumzika mkewe amerejea hospitalini ili kuendelea na matibabu kama alivyotakiwa na madaktari wake.

“Leo (jana) Mzee (Kingunge)  amerudishwa hospitalini tayari kwa ajili ya kuendelea na matibabu na amelazwa ICU (chumba cha wagonjwa mahututi) cha Mwaisela na hali yake inaendelea vizuri,” alisema Kinje.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment