Wednesday 25 January 2017

Simba Kutupwa Nje Kombe la Shirikisho..!!!.Fahamu zaidi hapa.

Klabu ya Simba huenda ikatupwa nje ya michuano ya kombe la shirikisho kufuatia kumpanga beki wake Novalt Lufunga kwenye mchezo walioshinda mabao 2-0 dhidi ya Polisi ya Dar es salaam huku akiwa na kadi nyekundu aliyoipata kwenye michuano iliyopita.
 Kwa mujibu wa rufaa ya klabu ya Polisi inadai kwamba Lufunga alilimwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa mwisho wa michuano hiyo msimu uliopita dhidi ya Coastal Union ya Tanga ambapo Simba ilitupwa nje ya mashindano.
 Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba Geofrey Nyange 'Kaburu' ambaye amelitolea ufafanuzi suala hilo huku akikanusha kuwa Lufunga hakucheza mchezo uliofuata baada ya ule wa Coastal, lakini pia akasema kuwa kanuni za mashindano hayo ni tofauti na kanuni za ligi.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment