Monday 30 January 2017

Trump Amtimua Kazi Mwanasheria Mkuu wa Serikali Baada ya Kupinga agizo lake la Kuwazuia Waislamu Wasiingie Marekanii.Fahamu zaidi hapa.

Rais wa Marekani Donald Trump amemfuta kazi kaimu mwanasheria mkuu Sally Yates saa chache tu baada ya kuwaagiza mawakili wa idara ya haki nchini humo kutotetea uamuzi wa kuwawekea vikwazo raia wanaotoka katika baadhi ya mataifa ya kiislamu.
 
Taarifa ya Ikulu ya Whitehouse imemshtumu kwa usaliti.
 
Sally Yates ambaye aliteuliwa na Obama alisema kuwa hafikirii kwamba marufuku hiyo ya muda kwa raia wa mataifa saba ya Kiislamu ni halali.
 
Wadhfa wake umechukuliwa na kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya kijimbo huko Virginia Dana Boente.
 
Agizo hilo la rais lililotiwa saini Ijumaa iliopita limesababisha maandamano nchini Marekani na ughaibuni.
Awali kundi moja la wanadiplomasia liliandika barua likikosoa agizo hilo wakisema litazidi kuhatarisha usalama wa taifa hilo.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment