Saturday 28 January 2017

Harmo Rapa Ang'ang'ania Jina la Harmonize ,Atoa Sababu Hizi Nzito za Kufanya Hivyo..!!!..Fahamu zaidi hapa.

Msanii wa bongo flava ambaye ndiyo anaanza kuchipukia, Harmo Rapa, amesema kuwa hana mpango na wala hawezi kubadili jina hilo lililompa umaarufu kwenye muziki kwa hofu ya kupoteza mashabiki wake. 
Msanii huyo anatamba na ngoma yake inayokwenda kwa jina la 'USIGAWE PASI'. ametoa msimamo huo kupitia eNewz ya EATV iliyomtafuta kuzungumza naye kuhusu mpango wa kubadili jina lake na kutotumia jina la 'Harmo Rapa'.
“Mimi sina mpango wa kubadili jina langu kwa sababu naogopa kupoteza mashabiki zangu na ukiangalia kwa sasa jina la Harmo Rapa limeshakuwa kubwa na tayari nimeshajitengenezea mashabiki kupitia jina hilo”
Pia amesema kuwa hana mpango wa kwenda WCB na wala hahitaji msaada wowote kutoka kwao huku akionesha jeuri kuwa angeweza kutoka hata bila kutumia jina hilo. "Hata bila kufananishwa na Harmonize mimi ningetoka tu"
Harmo Rapa ni moja kati ya wasanii ambao wamepata kiki ya kutosha kutokana tu na muonekano wake ambapo watu wengi wamekuwa wakimfananisha na Harmonize kutoka WCB.
Msanii huyo hivi karibuni katika kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio alijifananisha na Fid Q na kuwaacha watu midomo wazi.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment