Monday 30 January 2017

SIMU INAWEZA KUMTIA PAUL POGBA MATATANI, USHAHIDI HUU HAPA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Kiungo wa bei kubwa wa Manchester United, Paul Pogba anaweza kuingia matatani baada ya kuonekana akiendesha gari huku akitumia simu kitu ambacho ni kinyume na sheria za uendeshaji gari nchini England.

Pogba ameonekana akiendesha gari lake aina ya ua Audi RS6-R lenye thamani ya pauni 85,000 alipokuwa akiwasili mazoezini kwenye Uwanja wa Carrington, Ijumaa iliyopita.

Picha zimemuonyesha akiwa ameishika simu yake hiyo huku akiendesha gari na kama mamlaka husika za usalama barabarani zitaamua kutumia picha hiyo zinaweza kumuingiza matatizoni.
 
Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment