Sunday 22 January 2017

Huyu Kikwete Huyu,Tazama Hapa Jinsi Alivyowaweka Mtu Kati Mabilionea Dangote na Bill Gates na Kuteta Nao..!!!..Fahamu zaidi hapa.

Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amepata nafasi ya kukutana na mabilionea wawili wakubwa duniani akiwa ziarani Davos nchini Uswisi.

Rais Jakaya Kikwete alikutana na  tajiria namba moja Afrika, Alhaji Aliko Dangote  kutoka nchini Nigeria na tajiria namba moja duniani, Bill Gates kutoka nchini Marekani.

Viongozi hao wamekutana nchini Uswisi katika Mkutano wa Dunia wa Uchumi (World Economic Forum) wenye lengo la kujadili mustakabali na mwenendo wa uchumi wa dunia.

Mbali na masuala ya uchumi, mkutano au kongamano hilo pia hujadili kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo kwa sasa yamekuwa ni tishio kubwa kwa viumbe mbalimbali.

Mkutano huu huudhuriwa na viongozi kutoka mataifa mbalimbali pamoja na asasi nyingine za kuraia zikiwa na lengo la kuweka nguvu pamoja na kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment