Sunday 22 January 2017

Nyumba ya Mbunge wa CCM Yabambwa Kwa Wizi wa Umeme..!!!..Fahamu zaidi hapa.

SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) limebaini wizi wa umeme katika nyumba ya aliyekuwa Mbunge wa Mtwara Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hasnain Murji.

Mhandisi wa Tanesco Mkoa wa Mtwara, Fabiani Ruhumbika, alisema mita ya nyumba ya Murji ilibainika kuchezewa baada ya kuona umeme unaotoka kwenda kwa mteja ni kidogo.

Alisema matumizi ya mteja yanaonekana kuwa ni makubwa kuliko kiasi kinachotumiwa hali iliyowatia shaka kwamba kutakuwa na kuchezewa kwa mita.

Ruhumbika alisema kitendo cha mteja kupindisha mita kutoka kushoto kwenda kulia inaonyesha wazi kuwa ilipoteza kumbukumbu katika usomaji wake.

Mwakilishi wa mbunge huyo wa zamani, Mohamed Haji, alisema kitendo cha kubaini wizi huo hakijui kwa sababu yeye hana ufahamu wa masuala ya umeme.

Akizungumza mjini hapa jana, Mwenyekiti wa Ukaguzi wa Miundombinu ya Umeme kutoka Makao Makuu ya Tanesco, John Manyama, alisema wizi huo umekuwa ukilirudi
sha nyuma shirika hilo na kufifisha mipango yake ya kujiendesha.

Alisema ukaguzi huo ulibaini kuwapo na uchezewaji mita katika nyumba hiyo, huku kukiwa na vifaa vingi vinavyotumia umeme.

Manyama alisema wataalamu wa ukaguzi waligundua wizi wa umeme huo kutokana na kutumia vifaa vya kisasa vya kupimia bila kumwonea mtumiaji wa huduma hiyo.

Alisema mtumiaji anayekamatwa huanza kwa kukatiwa umeme katika mtandao wa Tanesco kisha wanapiga hesabu ili kujua wamepoteza kiasi gani cha fedha na kumtaka kulipa.

“Tumebaini kuwa watu wengi wanatumia umeme bila kulipa (wezi wa umeme) hatua inayosababisha shirika kuchukua hatua kwa kuwakamata na kuwapeleka katika vyombo vya sheria ili kuruhusu liweze kukusanya mapato halisi na kuwa katika hali nzuri ya utoaji wa huduma.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment