Thursday 21 January 2016

#YALIYOJIRI>>>Rais Dkt. Magufuli Amteua Jakaya Kikwete Kuwa Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam.Fahamu zaidi hapa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Chancellor of the University of Dar es salaam).
 
Rais Mstaafu Kikwete anachukua nafasi hiyo, iliyoachwa wazi na Marehemu Balozi Fulgence Kazaura aliyefariki dunia Februari, 2014.
 
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue Ikulu Jijini    Dar es Salaam, imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza tarehe 17 Januari, 2016.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam.
21 Januari, 2016.

0 comments:

Post a Comment