Friday 22 January 2016

#YALIYOJIRI>>>Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Atangaza Rasmi Tarehe ya Kurudiwa kwa Uchaguzi Mkuu.Fahamu zaidi hapa.

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imetangaza tarehe ya marudio ya uchaguzi visiwani humo baada ya matokeo ya uchaguzi uliopita kufutwa.

Uchaguzi huo sasa utafanyika Jumapili tarehe 20 Machi.
Tangazo hilo limetolewa  na mwenyekiti wa ZEC Jecha Salim Jecha.

Jecha amesema tarehe hiyo iliamuliwa na tume baada ya mkutano hapo jana.

"Uchaguzi huo utahusisha uchaguzi wa Rais, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani na hakutakuwa na uteuzi mpya wa wagombea wala mikutano ya kampeni," amesema Bw Jecha.

"Wagombea wote walioteuliwa hapo awali wataendelea kuwa wagombea katika uchaguzi huu."

0 comments:

Post a Comment