Thursday 28 January 2016

#YALIYOJIRI>>>Watu 30 Wameokolewa Baada ya Kivuko cha Kilombero Kupinduka Jana Usiku,Mtu Mmoja Hajapatikana Hadi sasa.Fahamu zaidi hapa.

Watu wapatao 30 wameokolewa mpaka sasa baada ya kivuko cha mto Kilombero kushindwa kuhimili upepo mkali ulioambatana na mvua ya radi  na  kukifanya kigonge nguzo za pembeni ya mto na kukosa mwelekeo hivyo kupinduka ndani ya maji jana usiku.

Kivuko hicho kilikuwa  na  watu 31  ambapo  mpaka sasa  mtu  mmoja bado hajapatikana.

Tukio la kivuko hicho cha mto Kilombero kushindwa kumudu upepo sio mara ya kwanza kujitokeza katika eneo hilo la mpakani mwa wilaya za Kilombero na Ulanga, ambapo juzi hali kama hiyo ilijitokeza.

0 comments:

Post a Comment