Tuesday 11 July 2017

Ajali ya ndege yauwa watu 16.

Mabaki ya Ndege yakiteketea kwa moto

Ajali hiyo ilitokea katika Kaunti ya LeFlore karibia kilomita 160 kusini mwa mji mkuu wa jimbo hilo, Jackson.

Kwa mujibu wa mtandao wa Shirika la utangazaji la Reuters Watu wote 16 waliokuwa ndani ya ndege hiyo waliangamia huku chanzo cha ajali kikiwa  bado hakijafahamika.

Hata hivyo jarida la kiserikali la  jimbo la Mississipi limeandika kuwa ndege hiyo ilianguka katika shamba moja na mabaki yake kutapakaa maeneo tofauti tofauti.

Ndege hiyo yenye namba KC-130 ni moja ya ndege za kijeshi zenye gharama kubwa zinazotumiwa na Jeshi la Marekani, kupitia ukurasa rasmi wa twitter wa Jeshi la Majini wamethibitisha taarifa hizo huku wakieleza kuwa taarifa zaidi zitatolewa kesho kuhusu ajali hiyo.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment