Gereza
kuu la Kigali maarufu 1930 lateketea kwa moto. kufikia leo jioni moshi
inaendelea kutanda. Kilichosababisha moto huo hakikajulikana.
Shughuli
za kuzima moto bado zinaendelea huku vikosi vya Askari Jeshi na polisi
vikionekana hapa na pale kando kando mwa jengo la gereza hilo.
Hilo
Ni gereza linalohifadhi wafungwa wa mchanganyiko wale wa kisiasa na
wengine wa mauaji ya kimbari. Miongoni mwa wafungwa wa kisiasa Ni
Victoire Ingabire aliyehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela miaka 4
iliyopita Kwa hatia ya kuchochea utengano wa kikabila na kuhatarisha
usalama wa raia.
Viongozi kadhaa serikalini wamefika kwenye eneo la tukio wakiwemo mawaziri na wakuu wa jeshi na polisi.
Bado
Ni mapema kujua athari zilizotokana na tukio hilo kwani waandishi wa
habari hawajaruhusiwa kuingia katika jengo la gereza kuu ya Kigali.
Magari ya zima moto bado yanapishana na magari ya kubeba majeruhi huku wafungwa wakionekana nje ya gereza na ulinzi ukiwa umeimarishwa.BBC
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
0 comments:
Post a Comment