Sokwe
amezalishwa kwa upasuaji wa dharura kusini Magharibi mwa Uingereza
katika sehemu uliyotengwa kwa kuhifadhia wanyama inayojulikana kama
Bristol Zoo.
Mama
na mtoto wa sokwe huyo wanaendelea vyema ,sokwe huyo alizaliwa kupitia
upasuaji usio wa kawaida baada ya mama yake kuonyesha ishara za ugonjwa
hatari wa shinikizo la damu.
Jopo
la kuongoza shughuli ya upasuaji kwa sokwe huyo liliongozwa na Profesa
David Cahill aliyeitwa kutoka hospitali ya kina mama NHS na mtoto wa
kike alizaliwa kwa oparesheni hiyo.
Kumekuwa
na sokwe wachache waliofanyiwa upasuaji wakati wa kujifungua
duniani,kisa cha hivi karibuni kikiwa kile cha San Diego Safari Park
mwaka 2014.
0 comments:
Post a Comment