Home »
Habari Moto
» Matokeo Ya Mtihani Kidato Cha Nne -2015 Yametoka,Yatazame Hapa.
Baraza
la mitihani Tanzania limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne
wa mwaka 2015 yanayoonesha kiwango cha ufaulu kushuka kwa asilimia 0.80.
Akitangaza
matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt Charles Msonde amesema
kuwa jumla watahiniwa 272,947 sawa na 67.53% ya watahiniwa wote
waliofanya mtihani wa kidato cha nne 2015 wamefaulu tofauti na mwaka
2014 ambapo ufaulu ulikuwa 68.33%.
Msonde amesema kwa upande wa watahiniwa wa shule, waliofaulu ni
240,996 sawa na asilimia 67.91 ya waliofanya mtihani, wasichana wakiwa
11,125 (64.84) na wavulana wakiwa 124,871 (71.09).
Amesema kwa upande wa watahiniwa wa shule, ufaulu umeshuka kwa asilimia 1.85 ikilinganishwa na mwaka 2014.
Aidha kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea, Dkt Msonde amesema
watahiniwa 31,951 sawa na asilimia 64.80 wamefaulu ikilinganishwa na
watahiniwa 29,162 (61.12) waliofaulu mwaka 2014.
Kwa upade wa ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata
watahiniwa wa shule, Msonde amesema waliopata daraja la kwanza ni 9,816
sawa na asilimia 2.77, daraja la pili ni 31,986 sawa na asilimia 9.01,
daraja la tatu ni 48,127 sawa na asilimia 13.56.
Aidha waliopata daraja la nne ni 240,996 sawa na asilimia 67.91 na
waliopata daraja la sifuri (waliofeli) ni 113,489 sawa na asilimia
32.09.
Watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa kati ya daraja la kwanza hadi la
tatu ni 94,941 sawa na asilimia 24.73 wavulana wakiwa 56,603 sawa na
29.99 na wasichana 38,338 sawa na asilimia 19.63.
Amesema kwa upande wa ufaulu wa masomo kwa watahiniwa wa shule,
ufaulu wa juu kabisa ni wa somo la Kiswahili ambapo asilimia 77.63
wamefaulu huku ufaulu wa chini kabisa ukiwa ni wa somo la Basic
Mathematics ambapo asilimia 16.76 wamefaulu.
Matokeo hayo yamepangwa katika mfumo wa madaraja (Division) badala ya
ule wa wasatani wa alama (GPA) kama ambavyo iliagizwa na Waziri wa
Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi hivi karibuni.
0 comments:
Post a Comment