Home »
Habari Moto
» #Breaking News>>>Waziri wa Afya,Ustawi wa Jamii Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewasimamisha kazi Wakurugenzi wanne wa Bohari ya Taifa(MSD).Fahamu zaidi hapa.

Waziri
wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu
amewasimamisha wakurugenzi wanne toka Bohari ya Dawa ya Taifa(MSD) kwa
ubadhilifu wa fedha takribani Shillingi Billion 1.5.
Ameyasema
hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika Kitengo cha Afya
ya Mama na Mtoto baada ya kupokea vifaa toka Bohari Kuu ya Dawa ya
Taifa (MSD), amesema amepata taarifa ya uchunguzi ofisini kwake ya
ubadhilifu wa kiasi hicho cha fedha na kuamua kuwasimamisha wakurugenzi
wanne kupisha uchunguzi.
“ Nimeletewa taarifa ofisini kwangu na
nimeamua kuchukua fursa hii kuwaambia na hili pia kwamba nimewasimamisha
wakurugenzi wanne toka Bohari ya Kuu Dawa ya Taifa kwa ubadhilifu wa
fedha na nisingeweza kusubiri nitumbuliwe mimi jipu na Mhe.Rais kwahiyo
nimeamua kuwachukulia hatua kwa kuwasimamisha kazi ili kupisha
uchunguzi kuendelea”
“ Hizi ni zama za kufanya kazi na kuwajibika
sasa inabidi tuwajibike kwa kufanya kazi na hatutowavumilia watendaji
watakaoenda kinyume na utaratibu katika ofisi yoyote ile katika sekta ya
afya na tutawachukulia hatua kwani tunataka uwajibikaji ili kuiendeleza
sekta ya Afya ambayo ni muhimu sana kwa kila mwanadamu” Alisema Ummy.
Amewataja
aliowasimamisha kazi kuwa ni Joseph Tesha Mkurugenzi wa Fedha na
Mipango, Misanga Muja Mkurugenzi wa Ugavi, Heri Mchunga Mkurugenzi wa
Manunuzi na Cosmas Mwaifani Mkurugenzi Kanda na Huduma kwa Wateja ambapo
amewataka Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Bodi ya Bohari ya Dawa ya Taifa
kuwaandikia barua mara moja ya kuwasimamisha kazi.
Katika
kuboresha sekta ya Afya nchini, Wizara wa Afya ,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee imejipanga kufanya kazi kwa taratibu na
misingi iliyopo ili kuhakikisha inapeleka mbele gurudumu la maendeleo
hasa katika sekta ya afya.
Related Posts:
#YALIYOJIRI>>>Picha:Nyumba mpya atakayohamia Rais Barack Obama baada ya kutoka White House.
Rais wa Marekani Barack Obama atapanga nyumba Washington, D.C baada
ya kuondoka katika Ikulu ya Marekani (White House) hapo mwakani ambapo
rais mwingine wa taifa hilo ataapa kushika madaraka baada ya Barack
Obama ku… Read More
#YALIYOJIRI>>>Ushindi wa Trump Waacha Kilio Bungeni Dodoma.Fahamu zaidi hapa.
Naibu
Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson amesema wabunge wanawake
wamesikitishwa na kushindwa kwa mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya
Chama cha Democrat, Hillary Clinton.
Dk. Tulia alitoa kauli hiyo bungeni mjini D… Read More
#YALIYOJIRI>>>Godbless Lema Arudishwa Rumande Baada ya Kunyimwa Dhamana Kwa Mara ya Pili.Fahamu zaidi hapa.
Ujanja
wa kisheria uliosababisha mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kukaa
mahakamani kwa saa 10, umemfanya kada huyo wa Chadema kukosa tena
dhamana.
Jana, Mahakama ya Hakimu Mkazi ilishatupilia mbali hoja za
S… Read More
#YALIYOJIRI>>>>Mahakama Yampa Siku 7 Profesa Lipumba na Msajili wa Vyama Kujibu Hoja za CUF.Fahamu zaidi hapa.
Mahakama
Kuu imewapa siku saba Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis
Mutungi na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na wenzake kujibu
madai ya chama hicho.
Msajili,
Lipumba na wenzake walipewa muda … Read More
UNAMJUA MKE WA DONALD TRUMP? NI MODO ILA MTATA KWELIKWELI.FAHAMU ZAIDI HAPA.Donald
Trump ndiye rais ajaye wa Marekani, ameshinda katika uchaguzi
uliofanyika wiki hii, matokeo hayo ni kama hayakutegemewa na wengi hasa
kutokana na aina ya maisha ya mteule huyo.
Trump
anajulikana kwa kuwa ni bilion… Read More
0 comments:
Post a Comment