Jeshi la Polisi Zanzibar limetoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa jeshi hilo linapanga kumkamata Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi, CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.
Taarifa zinazosambaa kwa kasi mitandaoni zinasema Maalim Seif anatakiwa kukamatwa kwa
tuhuma zinazohusiana na kujitangazia ushindi katika uchaguzi wa tarehe
25 Oktoba 2015 kama inavyoshinikizwa na Chama cha Mapinduzi Zanzibar.
Akiongea na mwandishi wa Dw, Issac Gamba, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi,
Kamishina Mkadam Khamis Mkadam, amesema yeye hajapata taarifa yoyote toka kwa wakubwa wake inayomtaka amkamate Maalim Seif.
Amesema jeshi la polisi ni taasisi kubwa inayohusisha viongozi mbalimbali, hivyo yaweza kuwa amri kama hiyo imetolewa kwa viongozi wengine
==>Zaidi, bonyeza hapo chini kumsikiliza
Amesema jeshi la polisi ni taasisi kubwa inayohusisha viongozi mbalimbali, hivyo yaweza kuwa amri kama hiyo imetolewa kwa viongozi wengine
==>Zaidi, bonyeza hapo chini kumsikiliza
0 comments:
Post a Comment