Tuesday, 23 February 2016

#YALIYOJIRI>>>Wakazi 16,000 wakosa huduma muhimu baada ya daraja kuharibiwa na Mvua.Fahamu zaidi hapa.

Wananchi  kumi na sita elfu wa kijiji cha Libango  wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wanakosa huduma muhimu baada ya daraja la Libango linalounganisha kijiji hicho na makao makuu ya halmashauri ya wilaya  ya Namtumbo kuharibiwa na mvua huku wakazi zaidi ya laki mbili wa wilaya ya Namtumbo wakikosa mawasiliano na kijiji hicho.
Wakazi wa kijiji cha Libango wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wanasema kuwa maisha yamekuwa magumu baada ya daraja hilo la Libango ambalo liko katika mto Lwegu  kuharibiwa  na mvua zinazoendelea kunyesha  kwani mawasiliano  kati ya kijiji hicho na makao makuu ya wilaya ya namtumboi yamekatika huku  vijana wakijipatia ajira ya kuwavusha watu kwa shilingi elfu mbili.
 
Afisa mtendaji wa kijiji cha Libango Bw.Christopher Ngonyani alinusurika kuzama kwenye mto Luegu ambapo ndipo pana dara la Libango wakati akijaribu kuvuka  katika mto huo ili awahishe  nyaraka za kiofisi kwenye ofisi za halamashauri ya wilaya ya Namtumbo.
 
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Bw.Chande Bakary Nalicho ametembelea eneo la tukio  na kupiga marufuku kuvusha watu kwa kutumia miti huku akisema watajenga daraja la muda wakati juhudi za kulijenga daraja hilo zikifanyika.

0 comments:

Post a Comment