Saturday, 13 February 2016

#MICHEZO>>>Hamisi Kiiza aipandisha SIMBA FC kileleni baada kuifungia timu yake.Fahamu zaidi hapa.

Timu ya Simba yapandishwa kileleni na mchezaji wake Hamisi Kiiza kwa Mabao mawili  Simba kileleni mwa ligi kwa mara ya kwanza baada ya kusubiri kwa misimu mitatu bila kukaa kileleni mwa ligi kuu Tanzania bara na kuacha ligi hiyo ikitawaliwa na mahasimu wao Yanga, Azam na Mtibwa Sugar ambao wamekuwa wakipokezana kuongoza ligi hiyo.
Kwa mara ya mwisho Simba iliongoza ligi mwanzoni mwa msimu wa 2013-14 wakati huo Simba ikiwa chini ya kocha Abdalah Kibadeni aliyekuwa akisaidiwa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na kuiongoza Simba kushinda michezo yake mitano ya mwanzo.

Bao la kwanza la Hamisi Kiiza lilitokana na pasi ya Mwinyi Kazimoto ambayo ilimkuta Kiiza aliyeachia shuti kali lililomshinda golikipa wa Stand United Frank Muwonge na kujaa moja kwa moja kambani.
Goli hilo liipa Simba nafasi ya kuongoza 1-0 mpaka dakika za kipindi cha kwanza kinamalizika huku Stand wakiwa hoi.

Kipindi cha pili Simba walipata bao la pili dakika ya 48 ikiwa ni dakika tatu tu tangu kipindi cha pili kuanza baada ya Hassan Kessy kumtoka beki wa kushoto wa Stand United na kuambaa na mpira kisha kutia krosi ambayo ilikwamishwa moja kwa moja wavuni na Hamisi Kiiza ‘Diego’.
Pastory Athanas aliipa Stand United bao la kufutia machozi dakika ya 89 baada ya walinzi wa Simba kujichanganya na kushindwa kuokoa mpira langoni mwao.
 Ibrahim Ajib (kushoto) akipambana na beki wa Stand United
 Nahodha wa Stand United Jacob Masawe (kulia) akimzuia Ajib
 Mwinyi Kazimoto (katikati) akisaidiwa kutoka nje na madaktari baada ya kuumia uwanjani.
Hassan Kessy akimwacha kwenye mataa Amri Kiemba.

0 comments:

Post a Comment