Spika
wa Bunge, Job Ndugai akiwatambulisha wabunge wa bunge la Afrika
Mashariki waliofika ofisini kwake leo katika ofisi ndogo za Bunge jijini
Dar es Salaam kwaajili ya kumpongeza kwa kuchaguliwa kuwa spika wa
bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa serikali ya awamu ya tano.
BUNGE la
Afrika Mashariki limesema kuwa changamoto zilizokuwepo katika Bandari ya
Dar es Salaam zimeweza kufanyiwa kazi na Rais Dk.John Pombe Magufuli na
kufanya Bandari hiyo kutoa huduma kwa ufanisi.
Hayo ameyasema leo Mwakilishi Bunge hilo, Shy Rose Bhanji wakati
Wabunge wa Afrika Mashariki Tanzania walipokutana na Spika Bunge, Job
Ndugai kwa ajili ya kufahamiana kutokana wabunge hao wanatokana na bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema kuwa Bunge la Afrika Mashariki lilikuwa walikuwa
wakizungumzia juu ya bandari ya Dar es Salaam katika utoaji uwa huduma
lakini sasa Rais Dk.John Pombe Magufuli ameweza kufanyia kazi.
Shyrose amesema wataendelea kutoa ushirikino kwa Rais katika kutumia farsa yake ya Hapa Kazi Tu katika kuwahudumia watanzania.
Nae
Mwakilishi wa Spika Owen Mwandumbimbya ambaye ni Afisa Habari wa Bunge
amesema kuwa Spika atatoa ushirikiano kwa wabunge kupitia kamati ya
Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.
Mbunge
wa bunge la Afrika Mashariki, Shy Rose Banji akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kufika katika ofisi
ndogo za bunge kwaajili ya kumpongeza Spika wa Bunge, Job Ndugai na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mbunge wa Bunge la Afrika, Shy
Rose Banji jijini Dar es Salaam leo katika Ofisi ndogo za Bunge.
0 comments:
Post a Comment