Jeshi
la Polisi Zanzibar limewataka madaktari kuacha kuwahudumia watu
wanaokwenda hospitali baada ya kupigwa na kikundi cha watu wasiojulikana
cha mazombi bila ya kuwa na fomu ya matibabu (PF3).
Akizungumza
na wanahabari mjini Unguja jana, Mkurugenzi wa Upelelezi Zanzibar, Salum
Msangi alisema matukio ya watu kujeruhiwa na kutopeleka taarifa polisi
yanachangia kuendeleza uhalifu.
Alisema taswira ya haraka
wanayoipata ni kwamba inawezekana watu wanaotendewa vitendo hivyo ni
wahalifu ambao wamekutana na wahalifu wenzao hivyo kuhofia kutoa taarifa
ili uhalifu wao usibainike hali inayosababisha kunung’unika pembeni
bila ya kufikisha taarifa maeneo sahihi ili zifanyiwe kazi.
“Kwa
mujibu wa taratibu zilizopo ni kwamba mtu yeyote anayefanyiwa kitendo
cha kihalifu anapaswa kutoa taarifa kwenye kituo cha polisi ili
uchunguzi au upelelezi ufanyike kubaini wahalifu hao,” alisema Msangi.
Alisema iwapo polisi itambaini daktari atakayetoa tiba kwa watu hao bila PF3 itamchukulia hatua.
Alisisitiza polisi kutowatambua mazombi
hao ambao huvaa soksi nyeusi usoni, wakiwa na silaha wanazotumia
kuwashambulia watu kwa vile wanaofanyiwa vitendo hivyo hawatoi taarifa.
Alisema kumejitokeza mambo matatu; vipeperushi vyenye vitisho, mazombi na kuwekwa alama za X kwenye
baadhi ya nyumba hasa Pemba na kutoa tahadhari kwa mtu yeyote
anayehusika, kikundi au jumuiya inayojihusisha na utoaji wa vitisho
hivyo kuacha mara moja kabla ya jeshi hilo kuchukua hatua kali dhidi.
Akivisoma vipeperushi hivyo, Msangi alisema kuna vikaratasi vimesambazwa vyenye ujumbe usemao ipo siku itakuwa kweli ‘One Day Yes’ kingine “Kutangazwa uchaguzi siyo kufanyika uchaguzi.”
0 comments:
Post a Comment