Mwanamkakati
wa aliyekuwa mgombea urais wa Zanzibar, Mohamed Sultan Mugheiry,
maarufu kwa jina la Eddy Riyami, amewekwa ndani na Jeshi la Polisi mjini
Unguja kwa tuhuma za kumtukana Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Eddy
Riyami ambaye ni mmoja wa wana mkakati wa timu ya ushindi wa aliyekuwa
mgombea urais wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, alikutwa na mkasa huo
jana baada ya kuitwa polisi kutoa maelezo kutokana na tuhuma
zinazomkabili.
Riyami
ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar, alikwenda
Polisi Makao Makuu kuitikia wito wa Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa
Makosa ya Jinai Zanzibar, SSP Simon Pasua, huku akiandamana na
Mwanasheria wa CUF, Masoud Faki Masoud.
Mwanasheria huyo jana alisema Riyami anatuhumiwa kwa kosa la matumizi mabaya ya kimtandao.
Alisema licha ya kuzikana tuhuma hizo, lakini Jeshi la Polisi bado lilimshikilia kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
“Ni
kweli ameshikiliwa na polisi kwa ajili ya kupitisha uchunguzi na yupo
Polisi Madema, eti Eddy kaambiwa kamtukana Dr. Shein kwenye ‘audio’
ambayo hata si sauti yake, lakini dhamana ipo wazi na tutamchukulia
dhamana,” alisema Masoud.
Akizungumzia
kukamatwa kwa Riyami, Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai,
Salum Msangi, alithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kwa ajili ya
uchunguzi zaidi.
“Kitu ninachoweza kuthibitisha ni kuwa tunamshikilia Riyami kwa ajili ya kupitisha uchunguzi,” alisema Naibu Kamishna Msangi.
Februari
15, mwaka huu Ofisi ya Mkurunzi na Makosa ya Jinai, ilimwandikia Riyami
barua ya wito na kumtaka kufika ofisi ya upelelezi iliyopo Makao Makuu
ya Polisi Zanzibar.
Riyami
alitii wito huo ambapo wiki iliyopita alikwenda lakini mmoja wa maofisa
wa Jeshi la Polisi aliyemwandikia barua alikuwa nje ya Zanzibar kwa
shughuli za kikazi na kumtaka kwenda jana jumatatu
Riyami
si mwanachama wa CUF, lakini mara kadhaa amekuwa akitumiwa na chama
hicho kwa ajili ya mikakati mbalimbali pamoja na ushauri.
0 comments:
Post a Comment