Mratibu
 Msaidizi wa Jeshi la Polisi, ASP Denis Mujumba, 39 ameieleza Mahakama 
ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa akiwa Mkuu wa Upelelezi Magomeni alimsikia 
Mbunge wa Jimbo la Ubungo Saed Kubenea akimwambia Mkuu wa Wilaya ya 
Kinondoni, Paul Makonda kuwa DC gani kibaka, mjinga, mpumbavu na cheo 
chenyewe kapewa.
ASP
 Mujumba aliyasema hayo  jana mbele ya Hakimu Mkazi, Thomas Simba wakati
 akitoa ushahidi wake katika kesi ya kutoa lugha chafu inayomkabili 
Kubenea dhidi ya Mkuu wa huyo wa Wilaya.
Akiongozwa
 na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa, Mujumba alidai 
kuwa baada ya Kubenea kuyatoa maneno hayo huku akionekana mwenye hasira,
 Makonda akiwa amesimama alishangaa, akakunja mikono yake na akawa 
anamsogelea Kubenea.
“Nikaona
 watarushiana ngumi, nikamsihi Mkuu wa Wilaya Makonda aondoke wakati huo
 watu walianza kushangilia huku wengine wakisikitika,” alidai shahidi huyo wa tatu wa upande wa mashtaka.
Alidai
 kuwa alimgeukia Kubenea na kumwambia kitendo alichofanya cha kutoa 
matamshi hayo ametenda kosa la jinai, akamkamata na kumpeleka kituo cha 
polisi Magomeni kwa mahojiano. 
Baada
 ya kutoa ushahidi huo, Wakili wa Kubenea, Peter Kibatala alimuuliza 
shahidi huyo kuwa ilikuwaje hadi Kubenea akayatamka maneno hayo.
Akijibu
 swali hilo, Mujumba alidai kuwa ni baada ya Makonda kumnyima nafasi 
Kubenea ya kuzungumza na wafanyakazi waliokuwa katika mgomo kwenye 
Kiwanda cha Tooku Garments Co. Limited. 
Pia
 Wakili Kibatala aliuliza kwamba siku hiyo kulikuwepo na waandishi 
lakini alipataje picha za video na sauti kutoka kwa waandishi wa habari?
Mujumba: Ni kweli kulikuwepo na waandishi na kwamba niliwasiliana na waandishi hao ili wanipe ushahidi wa picha, sauti au video. Waandishi walinijibu kuwa hawana ushahidi huo.
Kibatala: je ulikwenda na askari wangapi?
Mujumba: nilikwenda na askari wanane au tisa.
Kibatala: wataje majina
Mujumba: Ni Sajenti Peter, PC Hamis, Joachim na Doel.
Kibatala: Shahidi hajui askari wake kwani anajua jina moja tu la mwanzo na hajataja wote.
Maswali haya yalisababisha Mjumba kukunja sura na kutoa sauti ya juu huku akitaka kubishana, Hakimu Simba alimtaka aache kubishana
Wakili Kibatala kwa kutumia sheria Namba 155(a) aliiomba mahakama kuonesha picha za ushahidi zilizokuwa zianonesha hali halisi ya tukio.
Wakili huyo aliinesha mahakama picha ambazo zilionesha kuwepo kwa askari walioshika bunduki na kumzingira Kubena, kwenye picha hiyo Mujumba hakuwemo.
Hapo awali Mujumba aliieleza mahakama kwamba yeye ndiye aliyemsihi Kubenea aende naye kwenye Kituo cha Polisi Magomeni, hivyo Wakili Kibatala aliongeza kuwa, kwa kutokuwepo kwenye picha ile Mujumba alitoa maelezo ya uongo.

Hakimu
 Mkazi hata hivyo, baada ya shahidi huyo kutoa ushahidi wake, Hakimu 
Simba alihairisha kesi hiyo hadi tarehe 15 na 16 Aprili mwaka huu. 
 
0 comments:
Post a Comment