Waziri Ummy Mwalimu akikagua utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli
pamoja na watumishi na vibarua wakihamisha nyaraka na makabrasha
mbalimbali kutoka kwenye jengo lililokuwa likitumiwa kama ofisi na
watumishi wa wizara hiyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametembelea hospitali ya Taifa Muhimbili kukagua utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli
la kuwataka watumishi wa wizara hiyo waliokuwa wakilitumia jengo la
Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto kuhamisha ofisi zao na kuliacha kwa
ajili ya matumizi ya wodi ya wazazi.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo katika hospitali hiyo, Waziri
Ummy amesema kuwa mpaka kufikia kesho tayari jengo hilo litakuwa
limeanza kutumika kwa kuwa watafanya kazi ya kuhamisha makabrasha ya
watumishi hao usiku kucha kuhakikisha agizo la Rais John Magufuli
linatekelezwa mara moja.
Picha mbalimbali zinaonesha Waziri Ummy Mwalimu akikagua utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli pamoja na watumishi na vibarua wakihamisha nyaraka na makabrasha mbalimbali kutoka kwenye jengo lililokuwa likitumiwa kama ofisi na watumishi wa wizara hiyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,Dar es Salaam.

0 comments:
Post a Comment