SERIKALI
imeendelea kupaa katika ukusanyaji wa mapato baada ya kukusanya hadi Sh
trilioni 1.79, ambazo imezipeleka katika huduma za jamii, ikiwamo
elimu, maji, miundombinu na miradi ya maendeleo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Servacius Likwelile alisema hayo jana wakati akitoa taarifa ya hali ya mapato kwa kipindi cha Februari mwaka huu.
Kamishna
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata alisema makusanyo
yameongeza kutoka Sh trilioni 1.2 Desemba hadi Sh trilioni 1.79 Januari.
Kabla ya Oktoba mwaka jana, makusanyo hayo hayakuzidi Sh bilioni 900 kwa mwezi.
Dk
Likwelile alitaja maeneo ambayo fedha hizo zimeelekezwa ni kwa Mamlaka
ya Elimu (TEA) iliyopewa Sh bilioni 23.078; Sh bilioni 18.7 zinatekeleza
utoaji wa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za awali, msingi hadi
kidato cha nne kwa ajili ya ada, chakula na ruzuku.
Aidha,
Sh bilioni 13 zimeelekezwa kwenye mikopo ya elimu ya juu na Sh bilioni
moja zitatumika kujengea uwezo walimu walio masomoni na wakufunzi wao.
Pia
Sh bilioni mbili zimeelekezwa kupanua udahili katika mkoa wa Dar es
Salaam kama Rais John Magufuli alivyoahidi katika mkutano wake na wazee
wa mkoa huo.
Dk
Likwelile alitaja maeneo mengine yaliyonufaika na fedha hizo na
shilingi kwenye mabano ni Mpango wa Maji Vijijini (bilioni 17.1),
maendeleo ya ujenzi wa barabara (bilioni 58.8), miradi ya umeme vijijini
(bilioni 20.2), reli (bilioni 2.034) Serikali za Mitaa (bilioni 4.5),
na Mahakama zimepatiwa Sh bilioni 12.3.
Aidha,
Dk Likwelile alisema ili kuwajengea uwezo walimu walio masomoni na
wakufunzi wao, Wizara imetoa Sh bilioni 1.65 kwa ajili ya mafunzo kwa
vitendo.
Kati
ya fedha hizo, wakufunzi wamepatiwa Sh milioni 431.6, walimu walio
masomoni wametengewa Sh milioni 249.2 kwa ajili ya vifaa vya
kufundishia, posho na nauli.
Alisema
kuwa fedha nyingine kati ya hizo, kiasi cha Sh bilioni 573.7 zimetolewa
kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa umma na ulipaji wa deni la taifa
kwa mwezi huu zimetolewa Sh bilioni 842.1 na mifuko ya hifadhi za jamii
Sh bilioni 81.13.
Aidha
kiasi kilichotolewa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo ni Sh
bilioni 166.2 huku Chuo kipya cha Sayansi ya Tiba kilicho katika hatua
ya ujenzi cha Mloganzila huko Kibamba, nje ya Jiji la Dar es Salaam,
kimepatiwa Sh bilioni 18 .
Kaimu kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alfayo Kidata akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es SalaamKatibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Tarishi Kibenga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata akifafanua kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam jinsi Mamlaka hiyo ilivyofanikiwa kukusanya mapato kutoka trilioni 1.2 kwa mwezi Disemba mpaka trilioni 1 na bilioni 79 kwa mwezi Januari
0 comments:
Post a Comment