Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Amos Makala walipokutana mjini Moshi kwa ziara ya ukaguzi wa miradi iliyo chini ya sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Mkuu wa Wilaya ya Same Bw. Herman Kapufi akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wanaofanya kazi katika kampuni ya Dott Services Limited inayojenga barabara ya Same-Mkumbara Km 96. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa wafanyakazi wa kampuni ya Dott Services Limited kuhusu madai yao ambapo ameagiza waanze kulipwa madai yao baada ya siku mbili.
wafanyakazi wa kampuni ya Dott Services Limited wakishangilia kwa furaha baada ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa kumtaka mkandarasi kuwalipa madai yao yote ifikapo Februari 26, mwaka huu.
Muoneano wa Jengo la Kituo cha Forodha cha pamoja (One Stop Border Post) kwa upande wa Tanzania lililopo Holili.
Ujumbe wa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ukielekea katika kituo cha pamoja cha forodha (One Stop Border Post) kwa upande wa Taveta nchini Kenya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akipata ufafanuzi wa namna ya kituo cha pamoja cha Forodha kinavyofanya kazi kutoka kwa Meneja Forodha kwa upande wa Taveta – Kenya Bw. Daniel Nyambaka.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiagana na
Meneja Forodha kwa upande wa Taveta – Kenya Bw. Daniel Nyambaka mara
baada ya kukagua kituo hicho.
SERIKALI
imesema iko mbioni kukamilisha mkataba maalumu wa ajira utakaotumiwa na
makandarasi wote nchini katika kuajiri watanzania wazalendo kwenye
miradi ya ujenzi inayosimamiwa na sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasilino.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema hayo
wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Mkumbara-Same yenye urefu wa Km 96
mkoani Kilimanjaro.
Amemtaka
mkandarasi Dott Services Limited kukamilisha hatua za mwisho za ujenzi
wa barabara hiyo na kulipa stahili zote za wafanyakazi kwa mujibu wa
mikataba.
“Nakupa
mwezi mmoja kukamilisha ujenzi uliobaki wa barabara hii pia hakikisha
kila mfanyakazi ambaye amemaliza mkataba wake analipwa stahili zake zote
kwa muda usiozidi siku mbili”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Prof.
Mbarawa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Same Bw. Herman Kapufi kufatilia
kwa makini madai ya wafanyakazi wazalendo ya malipo ya likizo, mafao ya
NSSF, malimbikizo ya mishahara, matibabu na mazingira magumu ya kazi ili
yalipwe sambasamba na madai mengine na hivyo kuondoa malalakimiko
yaliyopo na yanayoweza kujitokeza mara baada ya kukamilika kwa mradi.
“Kuanzia
sasa mameneja wa TANROADS wahakikishe kwenye ujenzi wa barabara na
miradi iliyo chini ya wizara hii kazi ambazo watanzania wanaweza
kuzifanya zisifanywe na wageni kwani hali hiyo huwanyima haki watanzania
wenye ujuzi wa kuijenga nchi yao”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Naye
Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) mkoa wa Kilimanjaro Eng.
Marwa Rubirya amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa kwa sasa km 1,020 za
mtandao wa barabara wilayani Same zinapitika na serikali imeanza
kuongeza kiwango cha barabara za lami Wilayani humo ikiwemo ujenzi wa
barabara ya Same-Kisiwani-Maore-Ndungu na Kihuriyo hadi Mkomazi.
Amemhakikishia
Waziri Prof. Mbarawa kwamba TANROADS itaendelea kuhakikisha barabara za
milimani wilayani Same ambazo ni sawa na asilimia 75 ya barabara zote
wilayani humo zinapitika wakati wote wa mwaka kutokana na umuhimu wake
kwa shughuli za kiuchumi.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Same Bw. Herman Kapufi amemuomba Waziri Mbarawa
kuzipandisha hadhi barabara za Hedaru-Vunta-Miamba Km 41.2,
Bangarara-Chome-Ikokoa Km 25.6, na Ndungu-Lugulu Km 8 ili zihudumiwe na
TANROADS kutokana na umuhimu wake kiuchumi na kijiografia.
Katika
hatua nyingine Waziri Mbarawa amekagua kituo cha pamoja cha forodha
kilichopo Holili (Tanzania) na Taveta (Kenya) na kuona shughuli za
usafirishaji na uchukuzi zinavyoendeshwa na kusisitiza umuhimu wa kituo
hicho kufanyakazi kwa kushirikiana ili kuongeza mapato kwa nchi za Kenya
na Tanzania.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
0 comments:
Post a Comment