Kiongozi wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda Kizza Besigye amekamatwa tena na maafisa wa polisi. Dr. Besigye amekamatwa alipokuwa akijaribu kuondoka nyumbani kwake.
Rais
Yoweri Museveni leo asubuhi aliongea na BBC na kusema kuwa
serikali yake iliamua kumpa kifungo cha nyumbani ili kuzuia vurugu
baada ya zoezi la kupiga kura na kutangaza matokeo.
Museveni
alieleza kuwa walichukua uamuzi huo baada ya kubaini kuwa Dk. Besigye
alipanga kutangaza matokeo yake mwenyewe ambayo sio ya kweli na
kuhamasisha wafuasi wake kufanya fujo, vitendo ambavyo havikubaliki.
“Walikuwa
wanataka kufanya fujo. Kwanza walikuwa wanataka kutangaza matokeo yao
wenyewe ya uongo. Pili walitaka kufanya fujo za kuharibu mali,” alisema Museveni.
Kadhalika,
Museveni alieleza kuwa serikali yake haina mpango wa kuweka ukomo wa
Urais nchini humo kwakuwa tayari Bunge liliona ni vyema kuwa na kipindi
kisichokuwa na ukomo. Hata hivyo, alisema kuwa hana mpango wa kufanyia
marekebisho katiba ya nchi hiyo ili aendelee kubakia madarakani.
“Hakuna mpango wowote. Hatujazungumzia hilo. Lilikuja kwenye baraza la mawaziri tukasema hapana, hakuna haja ya kuongeza,”Museveni anakaririwa.
Katika
hatua nyingine, Museveni ambaye anaiongoza Uganda tangu mwaka 1986,
amepinga ripoti za waangalizi zilizodai kuwa uchaguzi huo haukuwa huru
na haki.
Alisema
kuwa wanaotoa madai hayo kwa madai kuwa nguvu ya jeshi ilitumika zaidi
hawaijui siasa ya Uganda kwani wanasiasa wengi hawajakomaa kisiasa hivyo
wanaweza kuanzisha fujo muda wowote.
0 comments:
Post a Comment