Uongozi
wa Yanga umepanga kumshitaki Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya
Simba, Kasim Dewji kwa kudaiwa kuvujisha jezi za timu hiyo.
Yanga
inamshutumu Dewji kwa kuipatia jezi Kampuni ya Huduma za Simu ya
Vodacom Tanzania ambayo ilizitambulisha juzi katika hafla ya kukabidhi
vifaa vya michezo kwa timu za Ligi Kuu Bara kwa ajili ya msimu ujao wa
ligi hiyo.
Katika
hafla hiyo ya kukabidhi vifaa vya michezo kutoka kwa Vodacom ambao ni
wadhamini wa ligi hiyo, Yanga haikuwakilishwa na kiongozi yeyote yule.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum
Mkemi alisema jezi hizo zilizotambulishwa na Vodacom katika hafla hiyo
kuwa wameinunulia timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu ni
uongo.
Alisema
Vodacom haijawanunulia jezi hizo bali jezi hizo ni mali yao
walizonunuliwa na wadhamini wao wakuu Kampuni ya SportPesa kwa ajili ya
kuiwezesha klabu hiyo kujipatia fedha kwa kuziuza.
Yanga
ilizipeleka jezi hizo kwa Dewji ambaye ni wakala wa kuuza jezi nchini
kwa ajili ya kubandikwa nembo ya klabu hiyo pamoja na kuandikwa
maandishi ya wadhamini wao.
“Tumeshangaa
sana kuona jezi zetu hizo zinatambulishwa Vodacom wakati sisi tulikuwa
bado hatujazitambulisha kwa sababu tulitaka zitambulishwe na mchezaji wa
zamani wa Arsenal, Sol Campbell ambaye analetwa na SportPesa.
“Dewji
ametuvurugia mipango yetu kwa hiyo hivi sasa tunajipanga ili kuona ni
hatua gani tutazichukua na ikiwezekana kumshitaki Dewji kutokana na
kitendo chake hicho cha kutuhujumu,” alisema Mkemi.
Hata
hivyo, alipotafutwa Dewji ili aweze kulizungumzia suala hilo,
hakupatikana kutokana na simu yake ya mkononi kuita bila ya kupokelewa.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment