Zikiwa
zimebaki siku mbili nchi ya Kenya kufanya Uchaguzi Mkuu, Mjumbe wa
Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa amefunguka sababu kuu zinazofanya
amtetee na kumnadi mgombea Urais kupitia chama cha Jubilee Uhuru
Kenyatta kuwa ni kiongozi shupavu.
Lowassa
ambaye jana alishiriki katika mkutano wa chama cha Jubilee alisema kuwa
kuna watu wanauliza kwanini yeye pamoja na CHADEMA wanamnadi kwa kuwa
kiongozi huyo ni shupavu na mpenda watu.
"Kuna
watu wananiuliza kwanini mnamnadi Uhuru Kenyatta, nasema tena hadharani
bila aibu yoyote huyu ni kiongozi shupavu anayependa watu, anaweza
kuongoza watu wetu, lakini cha pili Uhuru Kenyatta anapenda Afrika
Mashariki akiingia madarakani ataturuhusu tuendelee kuzunguka zunguka
kwenye mipaka hii kama Namanga pale bila hata shida, la tatu ni kwamba
aliingia madarakani nchi ikiwa kwenye vita lakini amewapa suluhu
ameingoza nchi imekwenda taratibu na akafanikiwa" alisema Lowassa
Mbali
na hilo Lowassa alisema kuwa licha ya mambo yote hayo lakini bado
ukweli utabaki palepale kuwa Uhuru Kenyatta anapenda Demokrasia
"Tangu
Demokrasia ya vyama vingi Uhuru Kenyatta hajaleta shida ya aina yoyote,
siku moja nimeona kwenye TV yenu mama mmoja amemtukana mpaka matusi ya
nguoni lakini asubuhi Rais anasema nimemsamehe bure, nawaambia huyu
ndiye anawafaa, naondoka nikiwa na matumaini" alisema Lowassa
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment