Saturday 5 August 2017

Video: Ebitoke athibitisha kufunga ndoa na Ben Pol.

Baada ya msanii Shilole kutangaza kufunga ndoa wakati wowote, naye mchekeshaji kutoka Timamu, Ebitoke amedai kuwa anatarajia kufunga ndoa na mkali wa RnB Bongo, Ben Pol wakati wowote.
Akiongea na Bongo5 Ebitoke ameeleza kuwa moja ya malengo yake kwa sasa ni kufunga ndoa na msanii huyu pia kufanya naye kazi kwa ukaribu zaidi.

” Ben Pol ni mpenzi wangu na yupo katika harakati za kutimiza malengo yangu, ikiwemo kufunga naye ndoa na kufanya kazi naye pamoja na kusaidiana, ila siwezi kusema ndoa itakuwa lini ila ndo kwanza tupo katika malengo na mipango,” amesema Ebitoke.

Akaongeza” Hivyo vitu vitakuja kwa sababu tuna malengo na mipango hiyo kwa sababu yeye ni mwanaume na mimi ni mwanamke.”



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment