Tayari
Simba imerejea jijini Dar es Salaam kumalizia maandalizi ya mwisho
kabla ya mechi yake ya tamasha la Simba Day ikiivaa Rayon Sports, timu
bora kutoka Rwanda kwa kipindi hiki.
Tamasha
hilo linafanyika Jumanne na kazi itakuwa ngumu kwa Simba kwa kuwa Rayon
wako vizuri na mashabiki wa Msimbazi wangependa kupata ushindi wa
kwanza wa Dar es Salaam wakiwa na wachezaji wapya.
Hata
hivyo, kipa wa Simba, Aishi Manula anataka kutumia vizuri kila nafasi
atakayoipata kukaa langoni kwani anamuhofia Said Mohamed ‘Nduda’.
Wote
wawili Manula na Nduda wamejiunga na Simba hivi karibuni ambapo Manula
ametokea Azam FC na Nduda akitokea Mtibwa Sugar, wote tayari wapo
kambini Afrika Kusini.
Manula
alisema Nduda siyo kipa wa kumbeza kutokana na kiwango chake
alichonacho hivi sasa akiwa langoni ndiyo maana wote wapo Taifa Stars.
Alisema
anafurahia changamoto atakayokutana nayo ndani ya Simba akiwa na Nduda
na kipa mwingine Emmanuel Mseje aliyesajiliwa kutoka Mbao FC.
“Nina
kibarua kigumu cha kuhakikisha ninapata nafasi ya kucheza katika kikosi
cha kwanza na hiyo inatokana na kiwango kikubwa alichonacho mwenzangu
(Nduda).
“Ninahitaji kucheza kwa kujituma na kutumia vizuri kila nafasi nitakayoipata kudaka nikiwa katika kikosi cha kwanza.
“Lakini
tumuachie Kocha Omog (Joseph) kwani ndiye atakayeamua kipa gani mzuri
atakayekuwa anapata nafasi ya kucheza,” alisema Manula.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment