Friday, 11 August 2017

Waziri Mwijage Acharuka.......Avifunga Viwanda 10 kwa Kushndwa Kuendelezwa.

Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage, amesema serikali imeanza utekelezaji wa awamu ya kwanza ya kutwaa viwanda walivyopewa wawekezaji na kushindwa kuviendeleza huku viwanda vingine vikiwa chini ya uangalizi wa muda

Waziri Mwijage amesema hayo jana Mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kikao kilichojumuisha wawakilishi wa Wizara za Fedha, Tamisemi na Wizara ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu.

Amevitaja viwanda hivyo kuwa ni kiwanda cha korosho Lindi, Mgodi wa Pugu Kaolin, Mkata Saw Mills Ltd, Manawa Ginnery Co Ltd, Kiwanda cha Chai Dabaga, Tembo Chipboard Ltd, Kiwanda cha Nguo cha Kilimanjaro, Mang’ula Mechanical and Machine Tools co. Ltd na Polysacks cha Dar es Salaam.

Aidha, Mhe. Mwijage amesema serikali ambayo awali ilibinafsisha mashirika 341 ya umma ambayo yalijumuisha viwanda, mashamba, makampuni ya biashara, mahoteli na makampuni ya usafirishaji lakini kati ya  hayo, viwanda vilivyobinafsishwa vilikuwa 156 huku viwanda vinavyofanya kazi vizuri ni 62, huku viwanda vinavyosuasua vikiwa 28, wakati viwanda visivyofanya kazi vikiwa 56 na viwanda kumi vikibinafsishwa kwa kuuza mali moja moja.
==>Msikilize hapo chini


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment