Monday 7 August 2017

Video: Roma Afichua Siri ya Mrembo Aliyemkatikia Jukwaani.

Rapper Roma amefichua siri ya mrembo aliyemkatikia jukwaani katika show yake ya Dar Live kitendo ambacho kililalamikiwa na mke wake katika mitandao ya kijamii.

Roma amesema mrembo huyo alipandishwa jukwaani na mke wake baada ya kuona mrembo wa awali hafanyi vizuri katika uchezaji.

“One of interested story, huwezi amini yule baby aliyepanda kukatika wife ndiye aliyemleta jukwaani, mwanzo nilipanda na binti mmoja ambaye alisema anajua kucheza na anaweza akaperform vizuri ule wimbo, nilivyopanda naye hakuonyesha ushirikiano mzuri, namlazimisha akatike akawa anaona aibu,” Roma ameiambia Bongo5 na kuongeza.

“Sasa wife alikuwa kwenye ile show akamuona demu anakatika vizuri  akamwambia ebu nenda kacheze na shemeji yako, na yule akaja kaweuka kweli, kafanya shughuli mpaka wife akajutia uamuzi wake kwa nini alimtuma aje jukwaani, sema was nice show,” amesema Roma.

July 5 Mwaka huu mke wa Roma kwenye ukurasa wake wa Instagram alieleza kukerwa na kitendo cha mrembo huyo, “Kuwa Na Mume Msanii Wakati Mwingine Ni #Stress Nyie Acheni Tu Jamani!!!  Aaaf kuna vibinti ndiyo kama vinafanya makusudi Kama Huyu!!! Nilitamani Nipande Jukwaani Nikamshushe,” aliandika. VIDEO:


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment