Kesi inayowakabili viongozi wa nafasi za juu katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Selestine Mwesigwa imehairishwa mpaka Agosti 24 mwaka huu ambapo watarudishwa tena Mahakamani kusomewa mashtaka yao.
Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, Wilbard Mashauri, ambapo ndipo mashtaka hayo yalifunguliwa mara ya kwanza na kuendelea kusomewa mpaka sasa.
Hata hivyo, Wakili wa utetezi, Nehemiah Nkoko amedai kwamba inaonyesha vielelezo tayari vimeshafikishwa Mahakamani lakini upande wa mashtka unachelewesha kutolewa uamuzi.
Kwa upande mwingine, viongozi hao wanatuhumiwa na makosa mbalimbali yakiwemo ya matumizi mabaya ya madaraka waliyokuwa nayo katika uongozi wao pamoja na kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment