Jeshi
la Polisi August 15, 2017 limetoa tamko la kupiga marufuku Waendesha
Bodaboda kubeba watoto wenye umri wa chini ya miaka 10 na kwamba
atakayekiuka agizo hilo pamoja na mzazi aliyeruhusu mwanawe kubebwa
watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na faini, kifungo au
vyote viwili.
Kamishna
Msaidizi wa Polisi ambaye pia ni Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama
Barabarani, Theopista Malya, amesema kuwa watoto wamekuwa kwenye hatari
kubwa wakipandishwa kwenye Bodaboda na wakati mwingine waendesha
bodaboda hubeba watoto zaidi ya mmoja jambo ambalo ni lazima likemewe.
Aidha,
alisema kuwa Jeshi hilo limeandaa kipindi maalumu cha Radio
kitakachorushwa na Clouds FM kila siku ya Jumatano saa 2:00 Usiku kikiwa
na lengo la kuongeza elimu kwa waendesha Bodaboda katika kuzingatia
Usalama Barabarani pindi wanapofanya shughuli zao.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Mabalozi wa Usalama barabarani (TSA), John Seka alisema
kipindi hicho kitalenga kuwapa elimu waendeshaji wa bodaboda.
Pia, alitumia nafasi hiyo kuwataka wafuate sheria zilizowekwa na Sumatra ili waepukane na mkono wa sheria.
Paulina Shayo ambaye ni mwakilishi kutoka WAT Saccos alisema kuwa wanatoa mikopo kwa bodaboda na kwamba mikopo hiyo itawasaidia kuwa wamiliki halali wa vyombo hivyo.

Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment