Afisa Habari wa klabu ya Azam, Jaffar Iddi amefunguka na kukanusha
taarifa zinazoendelea mitaani kuwa kipa namna moja wa Azam FC, Aishi
Manula amesaini mkataba na klabu ya Simba na kudai kuwa mchezaji huyo
bado atabaki Azam FC.
Jaffar Iddi amesema hayo leo wakati akiongea na waandishi wa Habari
ambapo alikuwa akitoa picha jinsi klabu ya Azam itakavyoendeshwa sasa
kwa kusema saizi wao watatoa kipaumbele zaidi kwa wachezaji
wanaochipukia na kusema klabu hiyo saizi haiwezi haiwezi kutumia gharama
kubwa sana kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma katika usajili, huku
akisisitiza kuwa mazungumzo ya kuwabakisha Manula na Shomari Kapombe
yapo katika hutua nzuri.
"Nisema tu kwamba Aishi Manula, Shomari Kapombe mikataba yao inakaribia
kuisha lakini mazungumzo ya Aishi Manula na Shomari Kapombe yapo katika
hatua za mwisho kabisa na nisema tu yanakwenda vizuri. Aishi Manula
ataendelea kubaki Azam FC kilichobaki saizi tunategemea wakitoka Misri
basi tukamilishe taratibu zao na ninawatoa shaka kuwa Aishi ataendelea
kubaki Azam FC hata yeye wakati anakwenda Misri na timu ya taifa
aliongea na waandishi wa habari akisema
"Sitatoka Azam FC labda niende nje ya nchi nikacheze lakini kwa timu za
hapa nyumbani sitaweza kufanya hivyo" kwa hiyo kauli yake inaenda na
kauli ya klabu ni kweli alikuwa anazungumzwa kuwa anakwenda kwenye klabu
za hapa nyumbani lakini yeye mwenyewe ameweka wazi hilo" alisema Jaffar
Iddi
Mbali na hilo Jaffar Iddi amesema kikosi cha Azam FC hakitakwenda nchi
yoyote ili kupiga kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu mwingine wa
Ligi Kuu Tanzania Bara bali wao wataweka kambi hapa hapa nchini na kudai
watakuwa Chamanzi, huku akibainisha kuwa wao wataanza maandalizi ya
msimu mpya mwezi wa saba.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment