Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George
Simbachawene amewaonya wakuu wa mikoa na wilaya kutotumia vibaya
madaraka yao ya kukamata watu walio kwenye himaya zao.
Ametoa onyo hilo leo (Ijumaa) alipojibu maswali ya wabunge
waliotaka kufanyika marekebisho ya sheria inayowapa mamlaka wakuu hao ya
kuwakamata na kuwaweka ndani wananchi wanaowatuhumu kwa lolote.
Licha ya kubainisha kwamba sheria hiyo haina tatizo, waziri
amesisitiza: “Ukamataji unatakiwa ufanywe kwa mtu aliyetenda kosa la
jinai au anayehatarisha usalama. Isiwe kwa show-off tu. Na mhusika
anatakiwa kufikishwa mahakamani mara moja, asishikiliwe tu.”
Amesisitiza kwamba wakuu hao ni wawakilishi wa Serikali kwenye
maeneo yao, hivyo hawatakiwi kutumia vibaya madaraka waliyokasimiwa.
Katika siku za karibuni wakuu wa mikoa na wilaya wamekuwa
wakilalamikiwa kuwaweka watu kizuizini pasipo kuwa na sababu za msingi,
miongoni mwao wakiwamo waandishi wa habari.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment