Mashindano makubwa ya Mabara yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi hii leo
Urusi ikiwa ni kabla ya mwaka mmoja kufanyika kwa fainali za kombe la
dunia nchini humo.
Kuelekea Michuano hiyo Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulimwenguni (FIFA)
limewataka waamuzi wote watakaochezesha kusimamisha mchezo endapo
Mashabiki watatoa Lugha za kibaguzi wakati wa Mechi.
Wenyeji hawa wa michuano ya Mabara pamoja na Kombe la Dunia mwaka 2018
hawana sifa nzuri juu ya matendo ya kibaguzi uwanjani na mara nyingi
kumekuwa pakizuka vurugu za mara kwa mara kitendo kinacho sababisha FIFA
kuweka waangalizi wake wa masuala ya kibaguzi viwanjani.
Urusi iliyo katika kundi A, leo itajitupa uwanjani katika mchezo wa
ufunguzi kwa kuwakabili New Zealand wakati timu ya taifa ya Ureno
ikiwakabili Mexico siku ya Jumapili.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment