Nyosso
amesaini Kagera Sugar mkataba wa miezi 24, amesisitiza amebadilika na
sasa amekuwa mtu mwema lakini amepiga kijembe kwa kusema waliodhani
ameisha wakutane uwanjani waone uwezo wake.
Mapema
wiki hii Kagera Sugar chini ya Kocha Mecky Maxime ilimsajili Nyosso
akiwa ametoka kwenye adhabu ya kufungiwa miaka miwili kwa kosa la
kumdhalilisha aliyekuwa nahodha wa Azam FC, John Bocco. Wakati huo
Nyosso alikuwa akiichezea Mbeya City.
Wakati
Nyosso anafanya kitendo hicho katika mchezo namba 32 wa Ligi Kuu Bara
msimu wa 2015/16 kati ya Azam na Mbeya City kwenye Uwanja wa Azam
Complex uliopo Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, mechi hiyo,
Azam ilishinda mabao 2-1.
Nyosso
amesema anafurahia kumaliza adhabu yake na sasa anarejea uwanjani akiwa
amejifunza vitu vingi na hawezi kurudia kufanya vitendo vya
udhalilishaji.
“Nimefurahi
kujiunga na Kagera Sugar, nimerudi kupiga kazi na hivyo sitazungumza
kwa mdomo bali vitendo, hivyo mtu yeyote atakayetaka kuona uwezo wangu,
tukutane uwanjani.
“Muda
wote niliofungiwa adhabu ilikuwa ikiniumiza moyoni, sasa mimi ni mtu
mpya na nilikuwa nafanya mazoezi ya nguvu ndiyo maana nasema sasa ni
kupiga kazi tu.
“Namshukuru
Mungu kwanza kwa kuniwezesha kumaliza adhabu hii lakini kama unavyojua
mimi siku zote huwa siyo msemaji sana katika vyombo vya habari, mimi
kazi tu,” alisema Nyosso.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment