Chama cha ACT Wazalendo kimemkana Isihaka Karanda aliyedai kuwa ni mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Pwani ambapo juzi alitangaza kukihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapainduzi mbele ya Rais Magufuli.
Taarifa hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Mkoa wa Pwani, Mrisho Swagara alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani wameamua kumdanganya Rais Dkt Magufuli.
Kiongozi huyo wa ACT Wazalendo alisema kuwa Isihaka alikuwa ni mwanamchama wao wa kawaida ambaye hakuwa tegemeo kwenye chama hivyo madai kuwa alikuwa mwenyekiti mkoa Pwani si za kweli na kwamba ni propaganda za CCM dhidi ya chama hicho.
Rais Magufuli akizungumza na mamia ya wananchi waliojitokeza katika viwanja wa Mjini Kibaha, Isihaka alitangaza kukihama chama hicho ambapo alipokelewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole. Alipokuwa akitambulishwa, ilielezwa kuwa ni Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Mkoa wa Pwani ambapo yeye mwenyewe alikiri hilo na kusema hata kwenye uchaguzi mkuu alimchagua John Pombe Magufuli.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment