Wednesday, 21 June 2017

Yanga Yashtuka, Yaanza Kumwekea Ulinzi Msuva.

KLABU ya Yanga, imesema kuwa, inamlinda kiungo wake mshambuliaji, Simon Msuva dhidi ya watu wabaya wanaotaka kuharibu kipaji chake na kufuta ndoto zake za kufika mbali kisoka.
Yanga wamefikia hatua hiyo baada ya kuwepo kwa taarifa za klabu mbili kutoka Kaskazini mwa Afrika kuonekana kumuhitaji baada ya kuridhishwa na kiwango chake alichokuwa akikionyesha ametajwa kuwa mchezaji bora wa Simba msimu huu, alisema siku zote amekuwa akifuata utaratibu aliojiwekea katika mchezo wa mpira kwa kuwa amekuwa hapendi kuona akirudishwa nyuma na mtu atakayekuwa anataka kuchukua nafasi yake.

“Hii yote imetokana na suala zima la nidhamu na kujituma kwa sababu siku zote nimekuwa sipendi kuona nikivunja miiko yangu katika mchezo wa soka ambayo nimejiwekea, kwa sasa natakiwa niendelee kufanya zaidi ya nilipofikia ili nizidi kuwa bora.

“Unajua mimi ni mchezaji na sitakiwi kumuhofia mchezaji yeyote katika timu yetu, najua kuwa hivi sasa timu inafanya usajili kwa ajili ya msimu ujao, naamini ushindani wa namba utakuwa mkubwa ila niseme tu kwa upande wangu kama nitaendelea kuwa mzima basi sitakubali kupokonywa namba,” alisema Tshabalala ambaye pia ni mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu kwa siku za hivi karibuni. Timu hizo zinazotajwa ni Al Ittihad inayoshiriki Ligi Kuu Misri na Difaâ Hassani d’elJadid (DHDJ) iliyopo Ligi Daraja la Kwanza Morocco.

Charles Mkwasa ambaye ni Katibu Mkuu wa Yanga, amesema: “Hatuwezi kumzuia mchezaji kwenda kucheza soka kwingine hasa nje ya Tanzania, ila tunachotaka kuona ni kwamba huko anapokwenda anakuwa na maisha mazuri na si kupata matatizo na
kumpotezea malengo yake.

“Msuva anatakiwa na Klabu ya Al Ittihad ya Misri na DHDJ ya Morocco, lakini klabu hizo hazijaleta maombi yanayoeleweka mpaka tukakubali kumuachia mchezaji wetu, wanatakiwa kufuata utaratibu uliopo na si kufanya mambo kiujanjaujanja, hatupo tayari kuona mchezaji wetu anakwenda kupata matatizo kwingine,” alisema Mkwasa.
Omary Mdose,  Dar es Salaam


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment