Wednesday, 21 June 2017

Lissu: Kama ACACIA ni Wezi, kwanini Polisi Wamewapiga Mabomu Wananchi wa Tarime?.

"Tumeambiwa Acacia ni wezi, hawana leseni ya uchimbaji, hawajasajiliwa nchini. Wananchi wa Tarime walipoamua kuchukua hatua wamepigwa mabomu.

Kama Acacia ni wezi na hawajawahi kuwa na leseni kwa nini polisi wa Magufuli wanawapiga wananchi wa Tarime mabomu? Nani anayetetea wezi hapa

Nani mchochezi kati ya Rais aliyelia hadharani kuwa Acacia wezi, na mbunge wa Tarime aliyewaambia wananchi kuchukua hatua dhidi ya wezi hao?"

Tundu Lissu amehoji hayo baada ya Polisi kuanza kumtafuta John Heche kwa kuchochea wananchi wavamie Migodi ya dhahabu.

Akiwa bungwni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche alifunguka na kusema kwa kuwa Rais Magufuli kupitia ripoti ya pili ya mchanga amesema kampuni ya ACACIA ni feki na haipo basi yeye anawaambia wananchi wa jimbo lake wajiandae kuingia mgodini kuchukua kila kitu.

Heche alisema hayo bungeni na kudai kuwa atasimamia zoezi hilo na kuhakikisha kuwa ndege za kampuni hiyo zikitua mgodini kwa ajili ya kubeba madini basi zinapigwa mawe kwa kuwa wananchi wa jimbo lake la Tarime ambapo hiyo migodi ipo wameumizwa sana kusikia hiyo kampuni inayochukua mali zao ni feki na hewa.

"Kampuni ile ya ACACIA Rais amesema feki na hakuna 'formula' ya kukamata mwizi mlisema wenyewe, formula ya kukamata mwizi ni kupambana naye sisi hatutaruhusu madini yatoke pale ndege ikitua itapigwa mawe, magari yao tutayakamata kwanza tunawadai fidia nyingi kweli kweli pale Tarime. Mhe. Spika sisi tulitegemea Mhe. Rais aseme madini yasiondoke nchini mpaka mambo hayo yote yapitiwe, tutazuia mchanga madini yanaondoka. Rais amesema ACACIA ni mwizi wewe unataka utaratibu wa kukamata mwizi Tarime, sisi watu wetu wameumia sana na maji ya sumu, ng'ombe wamekufa, watu wamepigwa risasi kwa mujibu wa ripoti ya Waziri wa Nishati na Madini watu wa Tarime zaidi ya 64 wameuawa pale mgodini" alisema Heche

Mbali na hilo John Heche alisema kuwa kama serikali itamkamata kwa maamuzi ambayo atafanya basi Watanzania watajua kuwa serikali haipo tayari kupigana vita hii ya kupigania rasilimali za nchi hii, hivyo amewataka watu wa jimbo la Tarime wajiandae na kuanza maandalizi ya kupigania rasiliamali zao ili waone kama serikali itapeleka jeshi la polisi kulinda mali za wezi hao.

Kwa siku tatu mfululizo wananchi wa Tarime wamekuwa wakivamia Mgodi wa dhahabu usiku na mchana huku Polisi ikiwapiga Mabomu na kuwatawanya.

By Figganigga/Jamii Forums


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment