MBIO
za kuwania uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zimezidi
kushika kasi baada ya Ofisa wa juu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
Shija Richard kujitosa kuwania urais wa shirikisho hilo.
Shija
ambaye ni Meneja ndani ya Mamlaka ya Mapato Tanzania, amechukua fomu
hiyo leo Jumatatu katika ofisi za TFF Uwanja wa Karume, Dar es Salaam,
ingawa hakuzungumza lolote kwa maelezo kuwa muda wa kampeni bado.
“Ni
kweli nimechukua fomu kuwania urais wa TFF, wengi mtataka kujua mengi
kuhusu mimi na kwa nini nimejitosa katika nafasi hii, tuvute subira
wakati wa kampeni ukifika nitazungumza, ila kwa leo itoshe
kuuthibitishia umma kwamba nimechukua fomu ya urais,” alisema Shija.
Mgombea
huyo ana Shahada ya Uzamili katika masuala ya Sheria za Kodi na Utawala
kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, pia ana Stashahada ya Uzamili ya
Usimamizi wa Fedha kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dar es
Salaam na Stashahada ya Juu ya Uhasibu kutoka Chuo Kikuu cha Uhasibu
Arusha (IAA).
Pia Shija amehudhuria mafunzo mbalimbali ya uandishi wa habari na ameandikia magazeti mbalimbali hapa nchini kuanzia mwaka 1997.
Mgombea
huyo aliwahi kuitumikia Taasisi ya Kuzuia na Kupambaana na Rushwa
(TAKUKURU) kabla ya kujiunga na Mamlaka ya Mapato Tanzania. Kwa sasa ni
Mhazini Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA),
akiwa pia amepata kuongoza klabu mbalimbali za mpira wa miguu kwa ngazi
tofauti.
Mwaka
2008 alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya Chama cha Soka
wilayani Chato (CDFA), ambapo alisimamia usajili wa chama hicho kuelekea
kwenye uchaguzi ambao hata hivyo hakugombea. Pia Shija amepata kuwa
Katibu Mkuu wa Klabu ya Michezo ya Bukoba Veteran iliyopo mkoani Kagera.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment