KUENDESHA gari zuri la kifahari ni moja kati ya ndoto za binadamu wengi.
Tatizo huja kwenye uwezo wa kununua gari hilo. Lakini kwa wenye nazo
si tatizo, wanapata kilicho bora kwa kutumia fedha zao.
Katika hali isiyo ya kawaida, kampuni maarufu ya kutengeneza magari ya
kifahari zaidi duniani ya Rolls Royce, imezindua gari lake dogo aina ya
Rolls Rorce Sweptail linalouzwa Dola za Marekani milioni 13 sawa na Sh
bilioni 29 za Kitanzania. Wataalamu wa magari ya kifahari wanasema gari
hilo ndio la gharama kubwa zaidi kuwahi kutengenezwa duniani.
Rolls Royce ni moja kati ya kampuni za kwanza kutengeneza magari ya
kifahari na ambayo kipindi cha nyuma na hata mpaka sasa hutumiwa na
viongozi wakubwa duniani. Mara baada ya Uhuru, Mwalimu Julius Nyerere
alipewa gari aina ya Rolls Royce na Serikali ya Uingereza kwa ajili ya
matumizi ya kiserikali. Kwa ambao wamepata nafasi ya kutembelea
makumbusho ya taifa yaliyopo jijini Dar es Salaam, bila shaka watakuwa
wamepata nafasi ya kuona baadhi ya magari aina ya Rolls Royce
yaliyotumiwa na Serikali ya Mwalimu Nyerere
Gari hili jipya ambalo limewaacha midomo wazi watu wengi duniani ikiwamo
matajiri wenye ‘pepo la magari ya kifahari’ limetengenezwa baada ya
mteja binafsi ambaye hakutaka kutajwa jina lake kusema yupo tayari
kulinunua kwa ofa hiyo.
Rolls Royce walikataa kumtaja mteja huyo lakini walisema ni mtu mwenye
ukwasi usio na shaka na alikuwa ametoa kazi kwa kampuni nyingine
zimtengenezee ndege binafsi na boti ya kifahari kwa muundo ambao utakuwa
na mfanano na gari hilo jipya.
“Sweptail ni aina ya gari la kifahari zaidi na gharama kubwa kuwahi
kutengenezwa na kampuni yetu. Gari hili limetengenezwa kwa maombi ya
mteja binafsi,” anasema Giles Taylor mkurugenzi wa ubunifu wa kampuni ya
Rolls Royce Motor Cars.
Timu ya Rolls Royce ilifanya kazi kwa karibu na mteja huyo na
kutengeneza gari hilo ambalo linamuonekano kama Rolls Royce ya mwaka
1920 na 1930 ikiwa na sehemu za kuhifadhi vitu vya gharama vya mteja
huyo.
Gari hilo lina uwezo wa kubeba watu wawili na sehemu yake ya juu
imetengenezwa kwa kioo cha aina yake ambacho kinalifanya kuwa na
muonekano wa kipekee.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Kwa kiasi kikubwa Sweptail limetengenezwa kwa matairi ya aluminium na
kampuni hiyo imesema hakuna gari jingine walilowahi kutengeneza kwa
mfumo huo.
Kwa mujibu wa Rolls Royce Motor Cars, mteja alitaka gari hilo kuwa dogo
lakini la kisasa na lenye uwezo wa kubeba abiria wawili tu. Mbao aina ya
Macassar Ebony na Paldao ziliunganishwa na ngozi nyeusi na vionjo
vingine vya siri kunakshi muundo wa ndani wa gari hilo.
Kuna batani moja kubwa ya kubonyeza ambayo akibonyeza sehemu maalum
hufunguka ambapo huweza kuhifadhi briefcase yake. Batani nyingine
iliyopo kati kati kufugua sehemu ambayo anaweza kuhifadhi mvinyo wake na
ukaendelea kupata ubaridi.
Akiitambulisha gari hiyo nchini Italia, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Rolls
Royce Torsten Müller-Ötvös aliielezea Sweptail kama gari la aina yake
ambalo linaonyesha ni kwa kiasi gari kampuni yake inavyomjali mteja.
“Sweptail inaeleza kila kitu kuhusu kumjali mteja. Siku zote huwa
tunamsililiza mteja na kufanya kadiri ya matakwa yake ili kumfanya awe
sehemu ya bidhaa aliyokuwa akiitamani,” anasema
Moja kati ya jambo la kushangaza ni kuwa, magari yote ya Rolls Royce,
hutumia ngozi ya ng’ombe dume peke yake kutengenezea siti zake. Sababu
ni kuwa watengenezaji wake huepuka ngozi za ng’ombe jike kwa kuwa
zinaweza kuwa na mikwaruzo ambayo mara nyingi hupatikana wakati ng’ombe
jike akiwa ana mimba.
Gari moja hutumia ngozi za ng’ombe dume wanane ili kuweza kukamilika.
Ng’ombe dume ambao hutumika kutengenezea muundo wa ndani wa Rolls Royce
hufugwa sehemu maalumu barani Ulaya ambako hali ya hewa ni baridi kiasi
kwamba mbu hawezi kuishi na hivyo kuwafanya kutoa ngozi isyo na mkwaruzo
wa aina yoyote.
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment