Sherehe
ya kula nyama ya mbwa iliogubikwa na utata katika mji wa Yullin nchini
China imeanza licha ya ripoti za awali kwamba ilikuwa imepigwa marufuku
mwaka huu.
Sherehe hiyo hufanyika kila mwaka katika mkoa wa Guangxi.
Mapema mwaka huu ,wanaharakati walidai kwamba wafanyibiashara waliagizwa na mamlaka kutouza nyama ya mbwa.
Lakini
wamiliki wa vibanda vinavyouza nyama hiyo walisema hawajasikia lolote
kuhusu hatua hiyo kutoka kwa maafisa. Mnamo tarehe 15 mwezi Mei, maafisa
wa mji walithibitisha kwamba hakuna marufuku yoyote.
Siku
ya Jumatano, ripoti kutoka Yullin zilisema kuwa mbwa waliokufa
walionekana wakiwa wametundikwa katika ndoano za nyama katika vibanda
ndani ya soko la Dongkou ambalo ndio kubwa mjini humo.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment