Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob, leo Ijumaa 30 Julai 2017, amezindua kituo cha kisasa cha kukusanya kodi, ushuru na tozo mbalimbali katika eneo la Simu 2000 pamoja na Kuhamsisha wafanyabiashara,bodaboda na Abiria wa Mabasi madogo .
Hii itapunguza kero kwa wananchi wanaoishi maeneo ya karibu na eneo la Simu 2000, kulipa kodi, ushuru na tozo mbalimbali ambapo awali walilazimika kwenda Kibamba zilizopo ofisi za Manispaa ya Halmashauri ya Ubungo.
Kituo hiki kipya kinategemea kuwasaidia wakazi wa Sinza, Makurumla, Mburahati, Mabibo, Makuburi, Ubungo na maeneo yote ya karibu.
Aidha amewataka Halmashauri ya Ubungo, kuwalinda na kuwatetea Bodaboda dhidi ya TANROADS na JESHI LA POLISI kwa kusajili vituo vya kupaki pikipiki na bajaji na kuwapa namba za utambuzi kwakuwa Bajeti ya Halmashauri 2017/218, inawategemea kuwapatia Bodaboda na Bajaji kiasi cha shillingi Billioni 4 kama chanzo cha mapato.Wakiendelea kughasiwa Halmashauri itazikosa pesa hizo.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment