Urusi
imeonya kwamba italipiza kisasi hatua ya rais wa Marekani Barrack Obama
ya kuwatimua wanadiplomaisa 35 wa Urusi kufuatia tuhuma kwamba Urusi
iliingilia maswala ya uchaguzi wa Marekani kwa njia ya udukuzi wa
mitandaoni.
Obama amesema Urusi pia imekuwa ikiwadhalilisha maafisa wa Marekani.
Kwa
upande wake, rais mteule Donald Trump ambae mara kwa mara amekuwa
akizipuuzilia taarifa hizo za udukuzi, sasa amesema atakutana na wakuu
wa kiintellijensia wa Marekani ili kupata undani zaidi wa swala hilo.
Msemaji wa rais Vladmir Putin amesema kuwa hatua zitakazochukuliwa na Urusi zitaiathiri Marekani.
Hatahivyo
amesema kuwa Urusi itasubiri hadi rais mteule Donald Trump ambaye
amepinga tuhuma hizo za udukuzi atakapochukua mamlaka.
Urusi imekana madai yoyote ya udukuzi na kuvitaja vikwazo hivyo vya Marekani kama visivyo na msingi.
Siku
ya Alhamisi, Idara ya maswala ya kigeni nchini Marekani ilitangaza
kwamba mabalozi hao 35 kutoka Urusi pamoja na wasaidizi wao huko San
Fransisco hawatakiwi Marekani na kuwapatia wao na familia zao muda wa
saa 72 kuondoka nchi humo.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
0 comments:
Post a Comment