MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ametokea benchi jana na kuisaidia timu yake, KRC Genk kushinda 2-0 dhidi ya mahasimu wao, Gent katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji.
Genk ilikuwa inacheza kwa mara ya kwanza leo bila ya kocha wake Mbelgiji Peter Maes iliyemfukuza jana na ikafanikiwa kushinda.
Samatta
aliingia dakika ya 51 kwenda kuchukuaa nafasi ya mshambuliaji Mgiriki,
Nikolaos Karelisn wakati huo tayari Genk inaongoza 2-0 mabao ya Pozuelo
dakika ya 19 na Karelis kwa penalti dakika ya 26.
Maes ndiye
aliyemsajili Samatta Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na akamuamini haraka na kumpa nafasi kwenye
kikosi cha kwanza.
jana Samatta amecheza mechi ya 36 Genk,18 msimu
uliopita na 18 msimu huu na kati ya hizo, ni michezo 17 tu ndiyo
alianza, 10 msimu uliopita na saba msimu huu.
Mechi 19 kati ya hizo
alitokea benchi, nane msimu uliopita na 11 msimu huu, wakati nane
hakumaliza baada ya kutolewa, sita msimu uliopita na mbili msimu huu
huku akiwa amefunga jumla ya mabao tisa, manne msimu huu na matano msimu
uliopita.
Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Bizot, Castagne, Brabec,
Colley, Uronen, Ndidi, Heynen, Pozuelo/Susic dk89, Bailey/Trossard dk81,
Buffalo and Karelis/Samatta dk51.AA Gent : Rinne, Neto, Mitrovic
Saief/Verstraete dk66, Nielsen/Desmet dk66, Perbet, Simon Foket, Esiti.
Dejaegere) Gershon and Milicevic.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
0 comments:
Post a Comment